Orodha Ya Maswali Yanayoulizwa Mara Kwa Mara
e-Mrejesho ni mfumo wa kutuma na kupokea malalamiko pamoja na Maulizo kutoka kwa wananchi.
Ndio, unaweza kutuma lalamiko lako kwenye taasisi husika.
Ili uweze kutuma lalamiko unatakiwa kuwa na simu ya mkononi (smartphone au simu kitochi) / kompyuta / kishikwambi (tablet).
Unaweza kutuma lalamiko wakati wowote na mahali popote ila tu unatakiwa kuwa na mtandao mzuri kama unatumia Mobile App au tovuti.
Ndio, unachotakiwa kufanya ni kubofya msimbo (*152*00*46#) kisha utachagua tuma lalamiko.
Unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye tovuti ya emalalamiko (https://emalalamiko.gov.go.tz/), bonyeza sehemu iliyoandikwa e-Mrejesho App, pakua, na sanikisha (install) kwenye simu yako.
Ndio, unaweza kutumia Mobile App au tovuti kufungua akaunti yako ya eMalalamiko unachotakiwa ni kujaza taaarifa zako kwa usahihi ili uweze kupata mrejesho wa pale unapotuma lalamiko lako.
Hapana, huduma hii ni bure kabisa unachotakiwa ni kuwa na namba ya simu kwaajili ya kupata namba na mrejesho wa lalamiko lako.
Ndio, unaweza kutuma lalamiko bila kujulikana unachotakiwa ni kuchagua sehemu ya tuma lalamiko bila kujulikana kwenye tovuti au Mobile App.
Kuna njia 2 (mbili) za kujua lalamiko lako limepokelewa na kujibiwa au la!
a) Kwanza kwa kutumiwa ujumbe mfupi kupitia simu yako ya mkononi endapo ulitumia akaunti yako ya eMalalamiko / ulijaza taarifa zako / Msimbo.
b) Pili kwa kutumia Namba (ID) ya lalamiko kupitia tovuti ya eMalalamiko, Mobile App au Msimbo.